FANGASI ZA UKENI (VAGINA YEAST INFECTION)

Huu ni ugonjwa unaoshika nafasi ya pili katika kuathiri sehezu za siri za mwanamke katika kipindi cha balee. Ungonjwa huu una athiri sehemu za nje na ndani ya uke (intravaginal). Tafiti zinaonyesha asilimia 70-75% ya wanawake walio katika balee wanaweza kupata tatizo hili japo mara moja. Na zaidi ya asilimia 40% tatizo hili linaweza kujirudia (recurrent).

Ugonjwa huu wa fangasi unasababishwa na vimelea vinavyotambulika kwa jina la ‘candida albicans’ kwa asilimia 80-90%. Vimelea hivi ni kati ya aina ya vimelea vya kawaida vinavyo patikana katika uke ila vinapozidi au kuwa vingi kuliko kawaida ndio vinasababisha ugonjwa huu.

Dalili za ugonjwa

Ugonjwa huu umekuwa na dalili nyingi na kuna baadhi ya wanawake kwa sababu wamekuwa na tatizo hili mda mrefu wanaona ni jambo la kawaida. Baadhi ya dalili ni kama zifuatazo:

  • Kutokwa na ute mzito mweupe mithili ya maziwa ya mtindi.
  • Kuwa na muwasho mkali ukeni (Pruritus)
  • Maumivu sehemu za ukeni
  • Hisia za kuwaka kama moto ukeni (burning vagina sensation)
  • Maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa (superficial dyspareunia)
  • Kutokwa na harufu isiyo ya kawaida ukeni.

Sababu zinazopelekea wanawake kupata tatizo hili:

  • Matumizi yasiyo sahihi ya dawa za kuua bakteria (irrational use of antibiotics) mfano dawa za UTI nk.
  • Kujisafisha ndani ya uke (douching)
  • Maumbile tofauti kati ya mwanamke na mwanamke (anatomical difference)(sehemu ya haja kubwa kuwa karibu sana na sehemu ya mbele ya uke hivyo kupelekea wadudu wa mfumo wa chakula kuenea na kuingia sehemu ya mbele)
  • Kujamiana kwa kupitia njia zote mbili (anal & vagina sex)
  • Magonjwa ya zinaa (STI)
  • Ugonjwa wa kisukari (Diabetis)
  • Kipindi cha ujauzito: inaletwa zaidi na mabadiliko ya homoni.
  • Matumizi ya pombe ya kupindukia
  • Matumizi yasiyo sahihi ya pedi kipindi cha hedhi.
  • Msongo wa mawazo (stress)

Kinga ni bora kuliko tiba. Ili kuweza kuepuka matatizo haya ya fangasi, ni vyema kufanya yafuatayo:

  • Kuacha matumizi yasiyo sahihi ya dawa za kuua bakteria (antibiotics)
  • Kuacha kujisafisha ndani ya uke
  • Kunywa maji ya kutosha (sio chini ya lita 3 kwa siku)
  • Usikae na pedi mda mrefu wakati wa hedhi (badilisha baada ya masaa 4 au inapokuwa imejaa)
  • Kuacha kutumia vilainishi visivyo rasmi wakati wa kujamiana (sex) (mfano mate (saliva), mafuta nk.
  • Kuacha kuweka manukato ukeni au vitu vinavyosadikika kurudisha uke kuwa mdogo
  • Jikinge na magonjwa ya zinaa
  • Kama ni mjamzito au unatatizo la kisukari onana na daktari.
  • Pendelea kutumia dawa zinazoweza kurudisha bakteria wa mwili katika hali ya kawaida (PROBIOTICS)
  • Jenga kinga ya mwili wako kwa kufanya yafuatayo:
    • Kula mlo kamili (balanced diet)
    • Pata mda mzuri wa kupumzika
    • Fanya mazoezi
    • Punguza unywaji wa pombe ulio kithiri
    • Punguza msongo wa mawazo (stress)

Hitimisho: ni vyema kuonana na daktari ili kupata ushauri zaidi na kuweza kufanyiwa uchunguzi kama tatizo lako ni la mda mrefu. Pia utaweza kushauriwa juu ya matumizi ya dawa ambazo ni bora na zilizo hakikiwa kwa kutibu tatizo hili la fangasi. 

Tembelea channel yetu ya YouTube (https://www.youtube.com/channel/UCYXDAMRKE2YW6GC5BO7GQYA) kupata elimu zaidi

Share na Wengine

5 thoughts on “FANGASI ZA UKENI (VAGINA YEAST INFECTION)”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Appointment

Make appointment here