TAMBUA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI(MENSTRUATION)

Hedhi, ni kipindi ambacho msichana/mwanamke katika umri wa balee anakuwa anatokwa na damu ukeni kama ishara ya mfumo wa uzazi kuwa upo kamilifu. Katika mambo yanayo wapa changamoto wanawake ni maswala ya hedhi/menses. Kuna wanawake wanamatatizo ya hedhi lakini wao wanaona kawaida kwa sababu wamekuwa katika hali hiyo mda mrefu sana hivyo imekuwa kama ni sehemu ya maisha yao.

NINI CHANZO KINACHOFANYA MTOTO WA KIKE KUPATA DAMU YA HEDHI?

Kuna muingiliano wa mfumo wa homini (hormones) ambazo chanzo chake ni tezi (Hypothalamus & Pituitary gland) zilizopo kwenye ubongo. Tezi hizi zina uwezo wa kutoa homoni mbali mbali baadhi ya hizo homoni (follicle stimulating hormones & Lutenizing hormoes) ndio zina peleka mawasiliano kwenye mifuko ya mayai (ovaries). Hii mifuko ya mayai ndio inazalisha homoni nyingine (estrogen & progesterone) ambazo ndizo zinazokuza ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi (endometrium) na matokeo yake kupata damu ya hedhi.

MZUNGUKO WA KAWAIDA WA MWANAMKE UNATAKIWA UWEJE?

Kawaida mzunguko wa mwanamke unatakiwa uwe kuanzia siku 21-35. Na asilimia kubwa mzunguko wa hedhini siku 28. Na ili kuweza kuzihesabu siku hizo unatakiwa kuweka kumbukumbu ya tarehe unayoanza kuona damu ya hedhi kwa mda wa mizunguko isiyo pungua mitatu (3). Hii ni kwasababu mabadiliko ya homoni yanaweza kusababisha mzunguko kuongezeka siku au kupungua.

HEDHI ZA MWANAMKE ZINATAKIWA ZITOKE KWA SIKU NGAPI (DURATION OF FLOW)?

Hedhi ya mwanamke inatakiwa kukaa kuanzia siku ya 2 mpaka siku ya 7. Hivyo damu yako ya hedhi kama itasita ndani ya siku saba tokea ilipoanzia hiyo ni yakawaida. Lakini pia uwingi wa hedhi unaweza kutuambia kwamba unamatatizo au hauna. Mfano: kwa mwanamke ambaye anapata ishara tuu kidogo (spot menses) na ikadumu ndani ya siku saba huyo anaweza akapata changamoto hata kwenye maswala ya kubeba mimba kwani ukuta unaotengenezwa sio mnene vya kutosha kuweza kushikilia mimba itakayotungwa.

DAMU YA HEDHI KI KAWAIDA INATAKIWA IWAJE?

Damu ya hedhi kikawaida inatakiwa iwe nzito kidogo na pia inaweza ikawa na vipande vipande (small clots) kidogo vya damu. Ila kwa kila mwanamke damu ya hedhi zinatofautiana. Ukitaka kujua kama damu yako ya hedhi ni ya kawaida unatakiwa kufanya mlinganisho na damu yako mwenyewe za siku za nyuma na sio kulinganisha na mwanamke mwingine. Ukiona inautofauti sana na hizo hedhi za nyuma basi ni vyema kuonana na doctor ili kupata ufananuzi zaidi.

Pamoja na hilo, unachotakiwa kujua zaidi ni kwamba, katika mwaka damu ya hedhi ikiwa inautofauti kati ya miezi 2 hadi miezi 3 haina shida kabisa ila inapoendelea kuwa tofauti sana basi hapo ni vyema kuonana na daktari ili kupata ushauri mzuri. Na utamrahisishia zaidi doctor wako kama ukiwa umeweka kumbukumbu za siku zako za hedhi ambazo hazikuwa sawa.

KIPIMIO GANI UNAWEZA KUTUMIA KUJUA UWINGI WA DAMU YAKO YA HEDHI?

Kawaida mwanamke anaweza kupoteza kiwango cha damu kuanzia 30mls mpaka 40mls. Kiwango hiki kimetajwa kuwa ni wastani tuu ila pia mwanamke akifikisha kiwango kisichozidi mls 80 bado ni cha kawaida. Kujua kiwango mwanamke anacho kipoteza kipimio ni mujumuisho wa pad anazotumia kwa siku. Mfano: Pad kama ALWAYS au HQ, ikiwa imejaa kabisa inaweza kubeba ujazo wa mls 12 wa damu ya hedhi. Lakini kama zitakuwa hazijajaa zinaweza kuwa zimebeba mls 5. Hivyo hivyo kwa wale wanao tumia tampoon, zenyewe zinaweza kubeba mls 5 mpaka mls 12 za damu ya hedhi.

JE MAUMIVU KIPINDI CHA HEDHI NI HALI YA KAWAIDA?

Kiwango cha maumivu kinautofauti mkubwa sana kwa kila mwanamke. kuna wanawake ambao hawana kabisa maumivu na kuna wale ambao maumivu huwa ni makali hata dawa za maumivu huwa hazifanyi kazi hivyo maumivu ya namna hii siyo ya kawaida. Maumivu ya kawaida ni yale ambayo ukitumia dawa unapata nafuu na unaweza kuendelea na shughuli zako za kila siku. Hivyo ni vyema kila mmoja kujichunguza yeye yupo kwenye kundi gani ili kupata kujua kama kuna haja ya kuonana na doctor kutokana na maumivu ambayo umekuwa nayo.

Share na Wengine

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Appointment

Make appointment here