SABABU ZA WANAWAKE KUKOSA HAMU YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

UTANGULIZI

Hamu ya kushiriki tendo la ndoa kwa wanawake huwa inabadilika mara kwa mara. Kunawakati inaweza ikawa ipo juu au chini na wakati mwingine kutoweka kabisa. Kwa mantiki hii, kama hapo awali ulikuwa huna tatizo na baada ya mda tatizo hili likaanza ni vyema kuonana na daktari kwa ushauri zaidi.

 

DALILI ZAKE

  • Kutotaka kujihusisha kabisa na maswala yanayohusu mapenzi ambapo hapo awali ulikuwa sawa
  • Kutokuwa na fikra zozote za kimapenzi
  • Kuanza kujiuliza maswali kwanini huna hisia wala kuwaza mapenzi.

SABABU

  1. Changamoto katika mahusiano:

Mara nyingi hamu ya tendo la ndoa huwa juu pale panapokuwa na mahusiano mapya au maelewano na mda mwingine kuwa chini au kutoweka kabisa pale mahusiano yanapopitia changamoto kama ugomvi wa mda mrefu au msongo wa mawazo kutokana na mambo yaliyoshindwa kutatuliwa.

  1. Mabadiliko ya mwili:

Baadhi ya mabadiliko ya mwili yanaweza kupunguza hii hali mfano;

  • kipindi cha ujauzito na wakati wa kunyonyesha: Kuna ongezeko kubwa la homoni ambapo baadhi ya wanawake inapelekea kukosa hamu ya tendo la ndoa
  • Ukomo wa hedhi (menopause): kipindi hiki homoni zinakuwa chini sana hivyo husababisha kupungukiwa na hamu ya tendo la ndoa na wakati mwingine kuisha kabisa.
  1. Ukavu wa ukeni:

Tatizo hili linaleta maumivu wakati wa SEX kutokana na ukosefu wa ute unaolainisha kuta za uke. Maumivu ya mda mrefu huwa yanasababisha mwanamke kukosa mhemuko wa tendo la ndoa.

  1. Maradhi/magonjwa ya mda mrefu:

Mfano wa magonjwa kama shinikizo la damu, kisukari, maaambukizi ya mda mrefu ya mfumo wa uzazi (PID)  na saratani (cancer). Matatizo haya kama hayajapata utatuzi sahihi yanaweza kuathiri saikolojia hivyo kukosa hamu ya tendo la ndoa

  1. Dawa “drugs”:

Tafiti zinaonyesha kuwa baadhi ya dawa (dawa za kupunguza msongo wa mawazo/antidepressants na dawa za kupanga uzazi za vidonge) zinaweza sababisha mwanamke akose hamu ya tendo la ndoa

NINI KIFANYIKE?

Usikae mda mrefu na hili tatizo hivyo nenda kwenye kituo cha afya ili uonane na daktari ambaye atabaini chanzo cha tatizo lako. Katika matibabu, kuna wanawake ambao watapewa ushauri peke yake na kuna wale ambao matatizo yao yanahitaji kutumia dawa ndio waweze kupata unafuu. Tukumbuke kwamba KINGA NI BORA KULIKO TIBA.

Share na Wengine

2 thoughts on “SABABU ZA WANAWAKE KUKOSA HAMU YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Appointment

Make appointment here