NINI CHA KUFANYA UNAPOJIKUTA UNATOKWA NA UCHAFU UKENI UNAO FANANA NA MAZIWA YA MTINDI UNAO TOA HARUFU MBAYA?

 

  1. Kama ni tatizo linalo jirejea mara kwa mara unatakiwa kuonana na daktari wako kwa uchunguzi wa kina.
  2. Unatakiwa pia kuangaliwa kama unaweza ukawa unadalili za saratani ya shingo ya kizazi.
  3. Ni vyema pia kuhakikisha unapima magonjwa ya zinaa kwani yanaweza kuchangia kutapa tatizo hili mara kwa mara.
  4. Unatakiwa kuchukuliwa maji maji ya ukeni ili yaoteshwe (HVS for culture) ili kutambua wadudu gani wanao changia kupata hili tatizo.
  5. Unatakiwa kuacha kutumia dawa ovyo (mfano antibiotics) ambazo hizi zinaweza kuchochea tatizo hili.
  6. Wahudumu wengi wa afya wanachanganya tatizo hili na tatizo linalojulikana kama PID. Hivyo waathirika wengi wanajikuta wakitumia dawa za kuua backeria (antibiotics) bila mafanikio yoyote. Ni vyema kutambua kwamba tatizo hili sio PID.
  7. Ni vyema kuacha kujisafisha ndani ya uke (douching) kwa nia ya kuweka mazingira ya ndani ya uke safi. Tatizo hili linawapata zaidi wale wanao jisafisha ndani ya uke na wengi wao wanapata mafundisho haya kwenye KITCHEN PARTIES bila kujua kujisafisha ndani ya uke ni kinyume na maadili ya afya.
  8. Wanawake wenye hili tatizo wanapaswa kutumia dawa zinaitwa PROBIOTICS (mfano: AVAFEM kidonge kimoja kila siku kwa miezi mitatu). Hizi dawa zinasaidia sana kurudisha bakteria wanao linda uke wako (normal vagina flora) na kukukinga wewe usipate matatizo haya ya ukeni.
  9. Tatizo hili kitaalamu linajulikana kama Bacterial Vaginosis na kikawaida sio tatizo kubwa au ugonjwa, ni hali inayojitokeza kwa sababu ya ongezeko kubwa la bakteria ukeni, hivyo moja kati ya tiba zake ni kutumia vitamins (Ascorbic acid 100mg mara 2 kwa siku kwa wiki 2). Nia ya vitamins ni kuwezesha mwini kupambana na bakteria).
  10. Unatakiwa kujitahidi kunywa maji ya kutosha kuanzia lita 3 kila siku. Ni vyema ukumbuke kwamba uke ni eneo linalotakiwa kuwa na unyevu nyevu na ndio maana mwanamke hawezi akakuta nguo yake ya ndani ipo kavu mda wote. Hii ni dhahiri kabisa kuwa uke unauwezo wa kujisafisha wenyewe. Kwa kuendelea kunywa maji ya kutosha utajikuta unapata unafuu mkubwa sana wa hili tatizo.
  11. Tabia nyingine za kuacha kuzifanya ni:
    • Kuacha kutumia vilainishi visivyo rasmi(mfano mate ya mdomoni au mafuta ya nazi) kama unakuwa mkavu sana wakati wa tendo la ndoa.
    • Kuacha kuweka dawa au vidonge vinavyo dhaniwa vinauwezo wa kubana uke wako.
    • Kuacha kuweka manukato kwa nia ya kutoa harufu mbaya uliyonayo.

HITIMISHO: Ukizingatia mambo yaliyo orodheshwa hapo juu na bila mafanikio yoyoye, usisite kuwasiliana nami kwa msaada zaidi.

Share na Wengine

2 thoughts on “NINI CHA KUFANYA UNAPOJIKUTA UNATOKWA NA UCHAFU UKENI UNAO FANANA NA MAZIWA YA MTINDI UNAO TOA HARUFU MBAYA?”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Appointment

Make appointment here