Mimba Zabibu (Molar Pregnancy)

UTANGULIZI

Mimba zabibu ni kati ya aina ya magonjwa ya mimba yanayoweza kujitokeza wakati seli za uzazi (mbegu ya mwanaume na mwanamke) kuungana na kutengeneza mimba isiyokuwa kamilifu. Tatizo hili hujitokeza kwa nadra sana lakini linaweza kuleta changamoto kubwa sana kwa muhusika. Tafiti zinaonyesha kutofautiana kwa ukubwa wa tatizo katika pande tofauti za dunia na pia wanawake wenye umri mdogo (chini ya miaka 20) na wale wenye umri mkubwa (juu ya miaka 40) ndio wako hatarini zaidi kupata tatizo hili.

AINA YA MIMBA ZABIBU NA CHANZO CHAKE

  1. Aina ya kwanza: Mimba zabibu iliyo kamilika (complete mole):
  • aina hii ya ugonjwa wa mimba ndio unao jitokeza zaidi ukilinganisha na aina nyingine.
  • Pia, aina hii kiumbe/mtoto  hatungwi (no fetal parts) bali kilichopo ni vipande vipande vya nyama vinavyofanania zabibu (placenta tissues).
  • Katika uchunguzi, aina hii huwa inatengeneza kiwango kikubwa sana cha homoni (beta HCG) kinacho sababisha kuwa na dalili za mimba zilizo pindukia.
  • Aina hii inatengenezwa pale mbegu ya kiume (sperm) inapo ungana na yai la mwanamke (ovum) lisilo kuwa na kiini chenye vina saba (nucleus) na kutengeneza ugonjwa wa mimba ulio na vina saba (DNA) vya baba peke yake
  1. Aina ya pili: mimba zabibu isiyo kamilika (Partial mole):
  • Aina hii ya ugonjwa wa mimba, unapofanyiwa uchunguzi unakuta zalio lina shida ila pia kiumbe/mtoto anaweza kuwepo.
  • Ongezeko la homini mwilini katika aina hii linaweza kuwa ni la kawaida na mwanamke anaweza akawa na dalili za mimba za kawaida.
  • Katika uchunguzi, vina saba (DNA) vya mama pamoja na vya baba vyote vinakuwepo katika katika aina hii.

DALILI YA MIMBA ZABIBU

Ugonjwa huu unaweza ukawa na dalili tofauti na zaidi huonekana kwa wale wenye aina ya kwanza ya mola (complete mole):

  • Dalili ya 1: Kutokwa na damu kipindi cha ujauzito
  • Dalili ya 2: Kuwa na dalili za mimba zilizo pindukia kipindi mimba bado ni changa mfano:
    • Kutapika sana kuliko kawaida
    • Kuwa na tumbo kubwa lisiloendana na wiki/miezi ya mimba.
  • Dalili ya 3: Kuongezeka kwa shinikizo la damu (high blood pressure)

MATIBABU YAKE

  • Ugonjwa huu unaweza kutibika na moja kati ya tiba inayotolewa ni kusafishwa mji wa mimba. Tiba zake zinakuwa na mafanikio makubwa kama tatizo hili litajulikana mapema. Pale tatizo linapo chelewa kujulikana, linaweza likaleta madhara makubwa kwa afya ya mama.
  • Tiba hii itaambatana na kufanyiwa Ultrasound na vipimo vya homoni za mimba (beta HCG) kabla na baada ya kusafishwa.
  • Katika kipindi cha matibabu utashauriwa usibebe mimba kwa mda usio pungua mwaka 1.

HITIMISHO NA USHAURI

  • Unapojihisi umebeba mimba, fika hospitali mapema kwa ajili ya vipimo.
  • Kumbuka kwamba, sio kila mwenye tatizo hili anakuwa na dalili na sio kila dalili inaashiria tatizo, hivyo njia sahihi ni kufanya vipimo.
  • Ugonjwa huu hauna kinga na kama ulishawahi upata upo na nafasi nyingine ya kuupata tena.
  • Ugonjwa huu usipo fanyiwa tiba sahihi unaweza ukabadilika na kuwa saratani (cancer) inayo julikana kama choriocarcinoma.
Share na Wengine

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Appointment

Make appointment here