JINSI AMBAVYO MAZIWA YA MAMA YANAWEZA KUMLINDA MTOTO NA UMANJANO

JINSI AMBAVYO MAZIWA YA MAMA YANAWEZA KUMLINDA MTOTO NA UMANJANO

Maziwa ya mama yanamchanganyiko wa virutubisho vingi vinavyoweza kupunguza tatizo la umanjano (Jaundice) kwa watoto wachanga. Jaundice/unjano, ni tatizo linalosababishwa na mkusanyiko wa kiwango kikubwa cha bilirubini kwenye damu ya mtoto. Bilirubini ni kati ya vitu vinavyo patikana ndani ya chembe hai nyekundu za damu (red blood cells-RBC) na ndizo zinazosababisha unjano wa ngozi kwa binadamu. Kunapokuwa na uvunjikaji wa chembe nyekundu (RBC), bilirubini zinaachiwa kwenye mzunguko wa damu kisha zinapitishwa na kufanyiwa kazi kwenye maini (liver) na baada ya hapo zinatolewa mwilini. Ila kwa baadhi ya watoto wachanga, maini yao yanakuwa hayajakomaa hivyo kukosa uwezo wa kuzibadilisha hizi bilirubin ili zitolewe nje ya mwili kiurahisi hivyo zinaishia kubaki katika mwili na kuleta hali ya unjano.

MUONEKANO WA MTOTO MWENYE UMANJANO

Maziwa ya mama yanaweza kupunguza unjano huu kwa njia zifuatazo:

  1. Kuupa mwili maji: asilimia kubwa (>80%) ya maziwa ya mama yametengenezwa na maji. Hivyo mtoto mchanga anapopewa maziwa ya mama kwa wingi inawezesha maini (liver) yake kufanya kazi vyema na kuweza kuziondoa hizi bilirubini kupitia njia ya mkojo na haja kubwa.
  2. Kolostramu (colostrum): Ni maziwa ya mama yale ya mwanzo ambayo ni mazito na yana rangi ya njano. Haya waziwa yanavirutubisho vinavyoweza kuupa mwili wa mtoto kinga juu ya magonjwa mbali mbali na pia yanaupa uwezo mwili wa kuvunja vunja na kuziondoa biliribun kwa kupitia njia ya mkojo na mfumo wa chakula.
  3. Mlo kamili: Maziwa ya mama yana virutubisho kamili vinavyowezesha ukuwaji mzuri wa mtoto. Mtoto anapopata virutubisho hivi kamili kwa njia ya maziwa, inawezesha mwili wa mtoto kuvunja vunja RBC kwa kiwango cha kawaida na kupelekea utengenezwaji mdogo wa bilirumini.
  4. Ulainishi wa choo: maziwa ya mama yanauwezo wa kulainisha choo na kuwezesha mtoto kupata choo vizuri. Kutokana na sababu hii, mtoto anaweza kutoa bilirubini mwilini na kupunguza nafasi ya kupata umanjano.
  5. Ngozi kuchukua mwangaza kiurahisi (light absorption): maziwa ya mama yana aina maalum ya kirutubisho (bilirumin isomer) chenye uwezo wa kunyonya (absorb) mwangaza unao tolewa wakati wa tiba ya umanjano na kupelekea urahisi wa kuvunja vunja bilirubini iliyo zidi mwilini.

Hitimisho:

Ni vyema kutambua umuhimu wa kumpa mtoto mchanga maziwa ya mama yake. Kwa kufanya hivyo tunamkinga mtoto juu ya magonjwa mbalimbali na kumwezesha awe katika nafasi ndogo ya kupata umanjano.

Share na Wengine

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Appointment

Make appointment here