JINSI YA KUEPUKA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

Maumivu kipindi cha kushiriki tendo la ndoa ni jambo ambalo limekuwa linajitokeza mara nyingi kwa wahusika ambalo limefikia mahala na kuathiri saikolojia ya wanandoa. Tatizo hili linapelekea wahusika kukosa hamu ya kushiriki tendo hilo na hatimaye kusababisha uaminifu kupungua katika mahusiano. Waanga wakubwa wa tatizo hili ni wanawake na ndio wanaopokea shutuma nyingi kutoka kwa wenzi wao.

Sababu kuu zinazopelekea kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa ni:

  1. Kuwa na ute kidogo ambapo inaweza kusababishwa na;
    • Kujisafisha mara kwa mara na vide ndani ya uke kwa maji au sabuni
    • Kujifukiza ukeni
    • Kuweka dawa zinazosadikika kubana uke
    • Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango kama sindano n.k
    • Tiba za mionzi kwa wale wenye saratani zilizo husisha mfumo wa uzazi
    • Unywaji mdogo wa maji.
    • Umri mkubwa (wale hedhi zao zilizofunga)
  2. Magonjwa na matatizo ya ukeni mfano:
    • Magonjwa ya zinaa kama kaswende
    • Magonjwa kama pelvic inflammatory disease (PID)
    • Fangasi za ukweni.
    • Uvimbe kwenye mfumo wa uzazi (uterine fibroids)
    • Kuwa na maumbile tofauti tokea ulivyozaliwa, mfano:
      • Vagina stenosis (uke kuwa mdogo kuliko kawaida)
      • Tight vagina hymen (kuta ya ubikra kuwa mgumu kupita kawaida)
      • Vagina atresia (kuzaliwa na uke usio kamilika au kutokuwa na uke kabisa)
  1. Misuli ya ukeni kuwa mepesi kukakamaa inapoguswa (vaginismus) na kusababisha maumivu

Kutokana na tatizo hili la maumivu katika tendo la ndoa kushamiri, kuwekuwa na tiba mbali mbali ambazo zinasadikika kusaidia tatizo hili. Changamoto ambayo ipo kwenye hizi tiba ni kwamba wahusika mara nyingi hununua na kutumia dawa zinazo tangazwa kupitia njia ya mtandao au wasambazaji bila kufika kwenye vituo vya afya na kupata ushauri ili kujua chimbuko la tatizo.

NINI KIFANYIKE?

Kumbuka, kinga ni bora kuliko tiba. Hivyo, kama wewe ni muhanga wa tatizo hili ni vyema sana kufika mapema kwenye kituo cha afya na kuelezea matatizo yako na kisha kupewa tiba sahihi. Na ili uweze kujikinga na tatizo hili ni vyema ufanye yafuatayo:

  • Kumbuka kuandaana vyema kabla ya tendo.
  • Kama kunajambo halijakaa sawa kwenye mahusiano liwekwe sawa ili kuepusha msongo wa mawazo.
  • Acha kabisa kujisafisha kwa kutia vidole ukeni kwa maji au sabuni
  • Acha kabisa Kujifukiza ukeni
  • Acha kabisa kuweka dawa zinazosadikika kubana uke.
  • Acha matumizi ya vilainishi (mfano: mate ya mdomoni, mafuta ya kupakaa, n.k) ambavyo havijathibitishwa na mamlaka husika.
  • Kama unatumia dawa za kupangilia uzazi onana na daktari umwelezee unaweza ukabadilishiwa dawa.
  • Kama upo kwenye tiba ya mionzi kwa wale wenye saratani zilizo husisha mfumo wa uzazi mwelezee daktari changamoto yako na utapewa maelekezo sahihi nini ufanye
  • Kunywa maji ya kutosha sio chini ya lita 3 kwa siku
  • Hedhi zako zikiwa zimefunga (menopause) onana na daktari kwa ushauri na utapatiwa dawa zitakazo kupa unafuu mkubwa.

Kama kutakuwa na maswali, wasiliana nasi.

Share na Wengine

4 thoughts on “JINSI YA KUEPUKA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Appointment

Make appointment here