Genital Prolapse (Kuporomoka kwa mfuko wa uzazi)

GENITAL PROLAPSE (KUPOROMOKA KWA MFUKO WA UZAZI)

Mfuko wa uzazi ni kiungo muhimu kwa mwanamke ambapo ndipo mimba zinapotakiwa kutunga na kukuwa. Lakini pia ni kiungo ambacho kimekuwa kikizongwa na magonjwa kadha wa kadha na kusababisha wanawake kufika hospitali kwa huduma tofauti. Matatizo ambayo yanajitokeza zaidi kwenye kiungo hiki muhimu ni kama; kutokwa na damu nyingi kipindi cha hedhi, kuota kwa uvimbe kama myoma (uterine fibroid), saratani ya uzazi na kuporomoka kwa mfuko wa uzazi.

Suala la kuporomoka kwa mfuko wa uzazi linaweza kujitokeza kwa mwanamke yoyote, lakini zaidi linaonekana kwa wale wanawake ambao wamezaa Watoto wengi. Kuna wanawake wachache ambao tatizo hili linajitokeza hata kama bado hawajazaa ( inamaanisha amezaliwa nalo). Hivyo hivyo, wanawake wengine wanapata pale ambapo hedhi zao zimesha potea (menopause).

Sababu kuu ambayo inapelekea kuporomoka kwa mfuko wa kizazi ni pale misuli (ligaments) zinakuwa zimeisha ule ukakamavu wake (kulegea kuliko kiasi) na kuchindwa kushikilia mfuko huo mahala pake.

Matibabu ya tatizo hili ni changamoto kwani njia ya uhakika ni kufanyiwa upasuaji na kurudishia mfuko huu mahala pake. Njia nyingine ni za mda mfupi ni kama vile kuwekewa rings ndani ya uke.

Unapokuwa na tatizo hili ni vyema kufika hospitali mapema na kuonana na mtaalamu wa matatizo ya kizazi na utapata utatuzi wa tatizo hili kwani linaweza kuchangia pia kuchelewa kupata mimba.

 

 

Share na Wengine

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Appointment

Make appointment here