About us

ABOUT US

Dr. Bernard Henry Kitange (CEO)

Blog hii imeanzishwa na Bernard Henry Kitange ambaye ni mbeba maono pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa uzazi aliyepo Tanzania. Kutokana na uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika kutoa huduma za afya hususani za mfumo wa uzazi,  ameona kuna mapungufu makubwa ya taarifa za afya kwenye jamii inayotuzunguka. Hivyo ameona kuwe na chombo ambacho kitatoa taarifa za afya hususani afya ya uzazi ambazo zitawafikia wanajamii kwa lugha inayoeleweka vyema kwao. Hivyo basi, maono yake makubwa ni kuona kila mwana jamii afike mahala pakuweza kujitambua na kupambanua matatatizo ya kiafya atakayokuwa anakutana nayo na kuweza kujua huduma gani anatakiwa aipate na wapi. 

Our Mission

Kuhakikisha jamii inapata maelezo sahihi kuhusu afya kupitia elimu itakayotolewa kwa lugha inayoeleweka. 

Our Vision

Kuhakikisha yakua kila mmoja wetu anafikiwa na kupata huduma bora za kiafya na kufahamu maendeleo ya afya pamoja na matatizo mbali mbali ya kiafya na ufumbuzi wake ili kutengeneza jamii ilio na uwelewa bora wa afya kwa maslahi ya kesho na baadae zaidi…

“Ni vyema kila mmoja wetu akaweka mkakati wa kutazama na kufahamu ubora wa afya yake kila baada ya mda maalum ikiwezakana alau kila mwaka kwa uchache wake."

Dr Kitange

Appointment

Make appointment here